Header Ads

Kenya Yamaliza Sensa Maalum Ya Wanyamapori


Shirika la Huduma kwa Wanyamapori nchini Kenya KWS limemaliza sensa maalum ya wanyamapori waishio katika mpaka wa Kenya na Tanzania.

Msemaji wa KWS Paul Gathitu amesema sense hiyo imefanywa kwa ajili ya kufahamu idadi ya wanyamapori, njia wanazopita, maji na rasilimali za nyanda za malisho, na kwamba ripoti kamili itatolewa mwezi ujao.

Naibu mkurugenzi wa KWS anayeshughulikia usimamizi wa ikolojia Shadrack Ngene amesema kazi hiyo itasaidia juhudi za kuwalinda Ndovu na wanyamapori wengine na kukabiliana na matishio mbalimbali kama vile shughuli za binadamu na mabadiliko ya hali ya hewa.

No comments

Powered by Blogger.