Header Ads

Kenya Yafanyia Majaribio Reli Ya Nairobi-Mombasa

Tokeo la picha la KRC Try SGR

Shirika la Reli ya Kenya KRC limeifanyia majaribio reli ya kisasa ya SGR na hali ya mabehewa ya abiria.

Wataalamu, abiria na viongozi wa Shirika hilo wamepanda treni hiyo ya majaribio kutoka Nairobi hadi Mtito Andei, na kuendelea hadi Mombasa.

Mhandisi wa reli hiyo Jeremiah Matu amesema kipande kutoka Nairobi hadi Mtito kimekamilika, na mfumo wake wa alama za elektroni umeanza kufanya kazi. 

Lakini mfumo huo kwenye kipande cha Mtito hadi Mombasa bado haujakamilika, na kazi inaendelea.

Mradi wa Reli ya SGR kutoka Mombasa hadi Nairobi umefadhiliwa kwa asilimia 90 na Benki ya Exim ya China, na asilimia 10 imegharamiwa na serikali ya Kenya.

No comments

Powered by Blogger.