Header Ads

Kenya Yaahidi Kurejesha Usalama Kwenye Wilaya Za Kaskazini

Tokeo la picha la Joseph Nkaissery

Kenya yaahidi kusambaza zaidi askari wa usalama katika wilaya za kaskazini zilizokosa usalama kutokana na wizi wa mifugo, mapigano ya kikabila na uvamizi wa mashamba ya mifugo.

Akiongea na wanahabari mjini Nairobi waziri wa usalama wa ndani Bw Joseph Nkaissery, amesema serikali itapambana vikali na vikundi vya uhalifu vinavyojihusisha na uvamizi wa mifugo, ujangili, na mauaji ya raia wa kaunti za Baringo, Elgeyo Marakwet na Laikipia.

Kauli yake imekuja baada ya mauaji ya Tristan Voorspuy raia wa Kenya na Uingereza yaliyofanywa Jumapili na wafugaji wenye silaha kwenye shamba la wanyama la Sosian, analomiliki yeye na mwenzake. 

Mapambano yaliyotokea kwenye shamba hilo la Kaunti ya Laikipia, ni ya karibuni zaidi kati ya wamiliki wakubwa na wafugaji wakigombea maji na malisho. Hata hivyo Bw Nkaissery amesema sababu kuu ya kuongezeka kwa migogoro hiyo ni ukame.

No comments

Powered by Blogger.