Header Ads

Juventus Wajiandaa Kumuuza Dani Alves

Tokeo la picha la Juventus  - sky sports
Mabingwa wa soka nchini Italia Juventus FC huenda wakakubali kumuachia kirahisi beki wao wa upande wa kulia Dani Alves ambaye anahusishwa na mpanga wa kuwaniwa na matajiri wa mjini Manchester (Man City).
Alves alijiunga na Juventus mwanzoni mwa msimu huu akitokea kwa mabingwa wa soka nchini Hispania FC Barcelona, na amekua muhimili mkubwa wa mafanikio ya Juventus kwa msimu huu.
Juventus tayari wameshajiandaa kuziba nafasi ya Alves endapo ataondoka kwa kuangalia uwezekano wa kumsajili beki wa kulia wa AC Milan Mattia Di Sciglio.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 24 anatajwa kuwa katika kiwango cha juu katika kipindi hiki, na huenda akauzwa kwa kiasi kikubwa cha pesa, endapo Juventus watatuma ofa ya kutaka kumsajili.

Mbali na Alves, Juventus huenda wakatoa ruhusa kwa beki mwingine Leonardo Bonucci kuondoka mwishoni mwa msimu huu, kufuatia sintofahamu ulioyoibuka kati yake na meneja Max Allegri.

No comments

Powered by Blogger.