Header Ads

Jeshi La Syria Latangaza Kukamata Mji Wa Palmyra Nchini Humo

Tokeo la picha la Syria Army

Jeshi la Syria limetangaza kutwaa mji wa Palmyra ulioko katikati ya nchi hiyo baada ya kupambana na kundi la IS na kulisababshia hasara kubwa. Sasa kikosi cha kutegua mabomu kinafanya ukaguzi mjini kote kwa kuondoa mabomu yaliyotegwa barabarani.

Taarifa iliyotolewa na jeshi hilo inasema ushindi huo ni muhimu kwa ulinzi wa utamaduni na historia ya mji huo mkongwe, pia ni sambamba na ushindi wa jeshi hilo mashariki mwa Aleppo.

Jeshi hilo limesema litaendelea kupambana na kundi la IS na makundi mengine ya kigaidi ili kurejesha usalama na utulivu nchini humo.

Mwezi wa Desemba mwaka jana kundi la IS lilishambulia tena mji huo miezi tisa baada ya kupoteza udhibiti wake kwa jeshi la Syria.

No comments

Powered by Blogger.