Header Ads

Innocent Shoo: China Inaweza Kuwa Taifa Namba Moja Kwa Uchumi Duniani


Wakati mkutano wa bunge la umma la China unaendelea na ripoti ya kazi ya serikali iliyotolewa na waziri mkuu wa China ikiendelea kujadiliwa, wanataaluma wa mambo ya uchumi na diplomasia wanaendelea kutoka maoni kuhusu ripoti hiyo.

Mtaalamu wa uchumi wa Chuo cha Diplomasia nchini Tanzania Innocent Shoo, ana mwelekeo wa uchumi wa China kwa sasa unaonyesha uwezekano kuwa katika mwaka 2035 hadi 2050 China inaweza kuwa namba moja kwa uchumi duniani. 

Bw. Innocent Shoo ameeleza kuwa sasa tofauti ya kiuchumi kati ya China na Marekani si kubwa sana. Lakini China imekuwa ikitoa vilevile mikopo nafuu kwa nchi za Afrika kupitia benki ya Exim ya China, hali inayoweza kusaidia kubadilisha upeo wa nchi nyingine za magharibi zinazopenda kuiga mfano wa China kwa nchi za Afrika.

No comments

Powered by Blogger.