Header Ads

Idris Aweka ‘Fumbo’ La Alichomfanyia Wema Sepetu Alipokuwa Selo Polisi

Aliyekuwa mpenzi wa mrimbwende Wema Sepetu, Idris Sultan ni mmoja kati ya watu wa karibu wa mrembo huyo ambao hawakuonekana kumtembelea alipokuwa mikononi mwa polisi hivi karibuni, lakini walifanya jambo.
Akizungumza hivi karibuni na Lil Ommy wa Times FM, Idris alieleza kuwa ingawa hakufika katika kituo cha kati cha polisi jijini Dar es Salaam kumuona Wema aliyeshikiliwa kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya, alifanya kile ambacho anaamini kilikuwa sahihi kufanya.
“Hiyo napenda kujibu kwamba nilifanya nilichotakiwa kufanya, ambacho ni sahihi kufanya na Wema anajua. Nadhani yeye ndio mlitakiwa kumuuliza ‘Idris alifanyaje’…” alifunguka.
Katika hatua nyingine, Idris alikanusha tetesi za kujisogeza kimahaba kwa Wema akieleza kuwa ukaribu wao ni wa kirafiki.
“Hatuna relationship (mahusiano) yoyote, ni washkaji tu. Siwezi kusema kwamba ni washkaji eti tutaonekana tuko close, hapana. Ni kama mara moja-moja tu utakuta kuna hiki na hiki, tumeongea mara moja au mbili…”
Wema alishikiliwa na jeshi la polisi kwa takribani siku saba baada ya kutajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwa miongoni mwa majina ya watuhumiwa wa dawa za kulevya.

No comments

Powered by Blogger.