Header Ads

DC Gondwe Ang'arisha Siku Ya Wanawake Handeni


Mkuu wa Wilaya akitazama moja ya bidhaa na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na akina mama katika kutengeneza Tanzania ya Viwanda.

Kikundi cha kinamama cha umoja ni nguvu wakiwa wamebeba bango lao
Wanafunzi shule ya msingi Msule wakisheresha kwa ngoma wakati wa maadhimisho hayo
Mkuu wa Wilaya Mh. Gondwe akajumuika kucheza na kinamama kusherehekea sikukuu yao
Moja ya kikundi cha kinamama wakipokea cheti cha utambulisho kutoka kwa Mkuu wa Wilaya.
Mkuu wa Wilaya akikata utepe kuashiria ufunguzi wa maonesho ya bidhaa za kinamama.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni (suti nyeusi), akiambatana na kundi la wamamama na wanafunzi siku ya maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani kwenye maandamano iliyofanyika kata ya Kwamgwe Wilayani Handeni.
Mh. Gondwe akihutubia wananchi siku ya wanawake ambapo alieleza Halmashauri kutoa kipaumbele cha mikopo kwa vikundi vya kinamama na kulinda watoto wa kike kuhakikisha wanamaliza masomo yao bila kukwamishwa. 

Diwani wa Kata ya Kwamgwe Bi. Sharifa Abebe akizungumza na wananchi wakati wa maadhimisho hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe akisoma moja ya bango la wanawake wa kikundi cha Umoja ni nguvu linaloonesha taswira ya mama aliebeba mtoto mgongoni, kichwani kabeba kuni na jembe na mkononi akiwa amebeba chakula huku mwanaume akiwa ameketi nyumbani kumngoja mama alietoka shamba aje kuandaa chakula.

Picha na Alda Sadango,Afisa Habari,wilaya ya Handeni

No comments

Powered by Blogger.