Header Ads

Chelsea Wawepa Somo Kabla Ya Kuwavaa West Ham Utd

Tokeo la picha la Westham UTD Vs Chelsea - sky sports

Wachezaji wa klabu ya Chelsea wametakiwa kugangamala endapo wanahitaji kufikia malengo ya kutwaa ubingwa wa England msimu huu.

Ombi hilo kwa wachezaji wa The Blues, limetolewa na meneja wao kutoka nchini Italia Antonio Conte alipokua akiwahusisa mikakati ya ushindi kuelekea kwenye mchezo wa ligi ya England dhidi ya West Ham Utd, ambao utachezwa baadae hii leo.

Conte amewaambia wachezaji wake kuhakikisha wanapambana wakati wote bila kukata tamaa, ama kuidharau timu pinzani.

Mtaliano huyo amesema endapo wachezaji wake wanataka kukumbukwa katika historia ya soka nchini humo, wanapaswa kuzingatia mambo hayo muhimu ambayo yataendelea kuwaongoza katika michezo inayowakabili wakianza na West Ham Utd usiku wa leo.

"Wachezaji wangu wote wana uwezo mkubwa wa kupambana, lakini linapokuaja suala la ushindani wanapaswa kuwa makini wakati wote kutokana na timu pinzani kuwa na mbinu ambazo zinaweza kutuondoa katika malengo yetu,"  Alisema Conte.

"Lakini jambo muhimu hapa ni kukumbushana kila inapobidi, ili kufanikisha azma ambayo tumesha ikusudia tangu mwanzo wa msimu huu.

"Hakuna jambo zuri kama kukumbukwa kwa kufanya vyema katika maisha yako, ndivyo ilivyo kwa wachezaji wangu, ninataka wakumbukwe kwa mafanikio watakayo yapigania."

Chelsea wanaongoza msimamo wa ligi ya nchini England kwa tofauti ya point saba dhidi ya Spurs, na kama wataendelea na moyo wa kupata ushindi mpaka mwishoni mwa msimu huu, watatawazwa kuwa mabingwa wapya wa England.

No comments

Powered by Blogger.