Header Ads

Bifu La Arsene Wenger Na Alexis Sanchez Hadharani

Tokeo la picha la Arsene Wenger and Alexis Sanchez
Siri ya mshambuliaji kutoka nchini Chile Alexis Sanchez kuanzia benchi wakati wa mchezo wa Arsenal dhidi ya Liverpool uliochezwa jumamosi imefichuliwa na gazeti la The Sun la England.
Gazeti hilo limeandika ukweli wa suala hilo ambalo lilionyesha kuwakera mashabiki wa Arsenal ambao walifuatilia mchezo huo uliomalizika kwa Liverpool kuibuka na ushindi wa mabao matatu kwa moja.
The Sun limeandika kuwa, meneja Arsene Wenger alishindwa kumtumia Sanchez katika kikosi cha kwanza, kufuatia mzozo ulioibuka kati yake na mshambuliaji huyo wakati mazoezi ya mwisho kabla ya kuelekea mjini Liverpool kwa ajili mchezo huo.
Wawili hao wamekua katika mzozo wa muda mrefu, lakini Wenger anapoulizwa hukanusha kuwepo kwa tofauti baina yao, jambo ambalo limeendelea kuidhinishwa na maamuzi anayoyachukua dhidi ya Sanchez.
Hata hivyo imedaiwa kuwa, Sanchez amepanga kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu na kwenda kusaka rizki mahala pengine itakapofika mwishoni mwa msimu huu.
Ugomvi wa wawili hao umedhihirika huku Arsenal ikiwa inaelekea kwenye mchezo mgumu wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya FC Bayern Munich utakaochezwa kesho katika uwanja wa Emirates jijini London.

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa mjini Munich majuma mawili yaliyopita, Arsenal walikubali kichapo cha mabao matano kwa moja, hivyo endapo watahitaji kusonga mbele watalazmika kupata ushindi wa mabao manne kwa sifuri na kuendelea.

No comments

Powered by Blogger.