Header Ads

Bartomeu Amkana Jorge Sampaoli

Tokeo la picha la Jorge Sampaoli Feb 2017Jorge Sampaoli

Rais wa FC Barcelona Josep Maria Bartomeu amewataka wadau wa soka duniani kuwa na subra katika suala la kumfahamu mrithi wa Luis Enrique, ambaye ataondoka mwishoni mwa msimu huu.

Bartomeu ameomba hali hiyo kwa wadau, kufuatia tetesi zinazoendelea kumuhusu meneja wa klabu ya Sevilla Jorge Sampaoli, ambaye anadaiwa kupewa kipaumbele katika kinyang’anyiro cha kumsaka meneja mpya huko Camp Nou.

Bartomeu amesema mpaka sasa uongozi wa FC Barcelona unaendelea na vikao vya ndani na haujafikia hatua ya kutambua nani atakuwa meneja wa kikosi chao.

Amesema ni mapema mno kuanza kutaja majina ya mameneja wanaowafikiriwa, kutokana na kila mmoja klabuni hapo kutambua umuhimu wa mapambano yanayoendelea uwanjani ya kuhakikisha wanatetea taji la ligi ya Hispania.

Sampaoli amekua akitajwa na vyombo vya habari kuwa mtu sahihi atakaeweza kuendena na mfumo wa FC Barcelona, baada ya kuonyesha umahiri mkubwa ukufunzi, tangu alipoanza kukinoa kikosi cha Sevilla CF mwanzoni mwa msimu huu.

No comments

Powered by Blogger.