Header Ads

Baraza La Usalama Lashindwa Kupitisha Azimio La Kuiwekea Vikwazo Syria

Tokeo la picha la UN

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshindwa kupitisha azimio la kuweka vikwazo dhidi ya Syria kutokana na tuhuma za matumizi ya silaha za kemikali.

Kwa mswada huo uliowasilishwa na Uingereza, Ufaransa na Marekani, nchi wanachama tisa zilipiga kura ya ndio, Russia, China na Bolivia zilipiga kura ya hapana, Kazakhstan, Misri na Ethiopia hazikupiga kura.

Baada ya upigaji kura, balozi wa China katika Umoja wa Mataifa  Liu Jieyi amesema, uchunguzi kuhusu matumizi ya silaha za kemikali bado unaendelea, ni mapema kwa sasa kutoa uamuzi wa mwisho.

Amesema baraza hilo linatakiwa kuunga mkono uchunguzi wa pamoja, na kutoa matokeo yake kwa usahihi, uhalisi na ushahidi imara. Ameongeza kuwa China inapinga matumizi ya silaha za kikemikali kwa nchi yoyote, shirika lolote na mtu yeyote katika hali yoyote.

Upigaji kura huo umefanyika wakati duru mpya ya mazungumzo ya amani ya Syria inaendelea huko Geneva.

No comments

Powered by Blogger.