Header Ads

Baraza La Usalama La Umoja Wa Mataifa Lalaani Shambulizi La Kigaidi Lililotokea Huko Kabul


Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani shambulizi la kigaidi lililotokea kwenye hospitali ya jeshi huko Kabul nchini Afghanistan, likisisitiza kupambana na ugaidi kwa nguvu zote.

Baraza la Usalama limetoa salamu za rambirambi kwa jamii wa watu walioathiriwa, watu na serikali ya Afghanistan, na linawatakia majeruhi wapone haraka.

Baraza hilo limesisitiza kuwa, aina zote za ugaidi ni tishio kali kabisa kwa amani na usalama wa kimataifa, na inapasa kuwaadhibu watekelezaji, wapangaji, wasaidizi na waungaji mkono wa vitendo vya kigaidi.

Kundi la IS limetangaza kuhusika na shambulizi hilo lililosababisha vifo na majeruhi watu zaidi ya 120.

No comments

Powered by Blogger.