Header Ads

Bakri Hassan Saleh Waziri Mkuu Mpya Sudan

Tokeo la picha la Bakri Hassan Saleh

Rais Omar al-Bashir wa Sudan amemteua makamu wa kwanza wa rais Bw Bakri Hassan Saleh kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa uamuzi huo, Bw Saleh atashika nyadhifa mbili za makamu wa kwanza wa rais na waziri mkuu wa nchi hiyo.

Msaidizi wa rais wa Sudan Bw Ibrahim Mahmoud Hamid amesema rais al-Bashir ametangaza uamuzi huo kwenye mkutano wa viongozi wa chama tawala cha Sudan NCP uliofanyika jana.

Kabla ya kuwa makamu wa kwanza wa rais mwezi Desemba mwaka 2013, Bw Saleh aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali za juu serikalini ikiwa ni pamoja na mkuu wa idara ya usalama, mshauri wa rais wa mambo ya usalama, waziri wa mambo ya ndani, waziri wa ulinzi na waziri katika ofisi ya rais.

No comments

Powered by Blogger.