Header Ads

Alikiba Atoa Sababu Ya Rapa M.I Kutoonekana Kwenye Video Ya Aje Remix

Msanii wa Bongo Fleva Alikiba, amerejea nchini na kupokelewa kwa shangwe na mbwembwe baada ya kutoka South Afrika kuchukua tuzo yake ya MTV Europe ambapo kwa mara ya kwanza tuzo hiyo alikabidhiwa Wizkid msanii toka Nigeria, katika shamra shamra hizo Alikiba aliandaliwa chakula cha jioni katika hoteli ya Double tree iliyopo jijini Dar es salaam, ambapo baadhi ya wasani walialikwa kushiriki chakula cha jioni na Alikiba akiwepo mwanamitindo Jokate Mwagelo na mchekeshaji Idris Sultan.
Katika hafla hiyo fupi msanii alikiba alipata nafasi ya kuhojiwa na baadhi ya waandishi wa habari, ambapo alizungumzia kuhusu video yake mpya ya Aje aliyoifanya South Afrika, mashabiki wengi walitegemea ujio wa video hiyo, M.I ambaye ni CEO wa label ya Chocolate city kutokosekana, lakini mambo yalikawa tofauti.
Alikiba alitoa sababu iliyomfanya M.I kutofanya video ya Aje  Remix kuwa ni mtu anayejali zaidi biashara zake.
”Hatukutaka kuingilia ratiba zake kwa hiyo sisi tuliweza kufanya ile ya kifaransa tukamaliza video. Lakini hii ya sasa hivi vile vile tulijitahidi kwa nguvu zetu zote kuhakikisha M.I atakwepo lakini kuna sababu ambazo sisi wenyewe, management yangu ziko nje ya uwezo wetu,” amesema kiba.
”Sababu tuliweza kukata tiketi mara mbili, namaansha siku mbili tofauti, licha ya kutumiwa tiketi kwa mara ya kwanza bahati mbaya akakosa ndege na siku ya pili tena ikakosekana ndege. Kwahiyo kibinadamu tu haipendezi, sio kwamba kuonesha tuna hela tumtumie tena tiketi ya tatu, hakunaga formula hiyo tukaona haina shida, we can do this,” amesema kiba.
King Kiba alimalizia kwa kusema ”Ndio maana nimeamua kufanya video ya utofauti ili nizibe pengo hilo”.

No comments

Powered by Blogger.