Header Ads

Afrika Kusini Yafuta Ombi La Kujitoa ICC

Tokeo la picha la Michael Masutha

Umoja wa Mataifa umethibitisha kuwa Afrika Kusini imeomba rasmi kutaka kufuta ombi lake la kujitoa mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC na kusimamisha utaratibu wa kujiondoa.

Tarehe 19, mwezi Oktoba mwaka jana, waziri wa mambo ya nje wa Afrika Kusini Bi. Maite Nkoana-Mashabane alisaini hati ya kuomba kujitoa ICC bila idhini ya bunge. 

Naibu mwenyekiti wa mahakama kuu ya jimbo la Gauteng Kaskazini amesema kitendo cha Bi. Mashabane ni kinyume na katiba, na kuamuru ombi hilo liondolewe.

Waziri wa sheria wa Afrika Kusini Bw. Michael Masutha amesema japo nia yao ya kujitoa imecheleweshwa na utaratibu wa kimahakama, uamuzi huo hautazuiliwa, na huenda bunge la nchi hiyo litajadili tena suala hilo.

No comments

Powered by Blogger.