Header Ads

Zlatan Ibrahimovic Ampa Simanzi Mama Pogba

Mshambuliaji kutoka nchini Sweden Zlatan Ibrahimovic usiku wa kuamkia leo alifunga hat-trick ya kwanza tangu alipojiunga na Man Utd mwanzoni mwa msimu huu, akitokea kwa mabingwa wa soka nchini Ufaransa PSG.
Zlatan Ibrahimovic alifunga hat-trick hiyo katika mchezo wa 32 bora ya michuano ya Europa League, ambapo Man utd walipambana na  Saint-Etienne ya Ufaransa kwenye uwanja wa Old Trafford.
Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Sweden alifunga mabao hayo katika dakika ya 15, 75 na 88.
Ushindi wa mabao matatu kwa sifuri unaiweka katika mazingira mazuri Man Utd kabla ya kuelekea nchini Ufaransa kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa pili, ambapo wapinzani wao watalazimika kusaka mabao manne kwa sifuri, endapo watahitaji kusonga mbele.
Mchezo wa jana uliwakutanisha kwa mara ya kwanza msimu huu ndugu wawili wanaocheza klabu tofauti Paul Pogba wa Man Utd na Florentin Pogba wa St Etienne.
Mama wa wawili hao Yeo Moriba, alikua kwenye wakati mgumu wa kufuatilia mchezo wa jana, ambapo alidiriki kusema angependa kuona matokeo ya sare, ili kuepusha simanzi kwa mmoja wa watoto wake.
Hata hivyo mambo yalikua tofauti na kwa sasa anaamini Florentin Pogba alilala akiwa na maumivu ya kupoteza mchezo.

Hali kama hiyo kwa Yeo Moriba itajirudia tena juma lijalo ambapo watoto wake watakutana tena kwenye mchezo wa mkondo wa pili wa 32 bora ya Europa League.

No comments

Powered by Blogger.