Header Ads

Yakubu Aiyegbeni: Nitastaafu Soka Nikiwa England

Tokeo la picha la Yakubu Aiyegbeni - sky sports
Aliyekua mshambuliaji wa timu ya taifa ya Nigeria Yakubu Aiyegbeni amefichua siri ya kurejea katika soka la England, akitokea Uturuki alipokua akiitumikia klabu ya Kayserispor.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 34, amerejea nchini England na kujiunga na klabu ya Coventry city inayoshiriki ligi daraja la pili.
Yakubu amezungumza na shirika la urtangazaji la Uingereza BBC na kusema: "Niliondaka na kuelekea nchi za China, Qatar na Uturuki, lakini familia na moyo wangu vilibaki hapa England.
"Siku zote ninaamini nitamaliza maisha yangu ya soka nikiwa katika ardhi ya England."
Yakubu aliweka historia ya kufunga mabao 96 alipokua mmoja wa wachezaji wa ligi ya nchini England, ikiwa ni idadi kubwa ya mabao dhidi ya wachezaji wengine kutoka Nigeria waliowahi kucheza kwenye ligi hiyo.

Maisha yake ya soka nchini England yalianza miaka 14 iliyopita na alizitumikia klabu za Portsmouth, Middlesbrough, Everton na Blackburn Rovers.

No comments

Powered by Blogger.