Header Ads

WFP Yapanga Kusambaza Chakula Kwa Watu Milioni 4.6 Nchini Sudan

Tokeo la picha la WFP

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP limetangaza mpango wa kusambaza chakula kwa watu milioni 4.6 nchini Sudan wakiwemo watu milioni 3.4 wa Darfur na milioni 1.2 wa maeneo ya Kati na Mashariki.

Shirika hilo limeeleza kuwa upatikanaji wa chakula nchini humo umeathiriwa na mgogoro, kuyumba kwa uchumi na mabadiliko ya hali hewa. Mambo hayo yamesababisha hali ya dharura iliyopo sasa, na kuchochea msukosuko wa watu kukimbia makazi yao.

Shirika hilo limefafanua kuwa matatizo ya kuyumba kwa uchumi na mabadiliko ya hali ya hewa, yamesababisha mfumuko wa bei na kuathiri vibaya bei ya chakula, ambapo kwa sasa mfumuko wa bei umeongezeka na kufikia asilimia 53 juu ya kiwango cha wastani wa miaka mitano.

No comments

Powered by Blogger.