Header Ads

Waziri Mkuu Wa Zamani Achaguliwa Kuwa Rais Mpya Wa Somalia


Waziri mkuu wa zamani wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo amechaguliwa kuwa rais mpya wa nchi hiyo baada ya kushinda uchaguzi waliokuwa na ushindani mkali uliofanywa huko Mogadishu.

Farmajo anayekuwa rais wa tisa wa nchi hiyo, alitangazwa mshindi baada ya rais Hassan Sheikh Mohamud anayeondoka madarakani kukubali kushindwa kwenye uchaguzi huo.

Farmajo aliongoza katika duru ya pili ya upigaji kura bungeni, lakini alishindwa kupata uwingi wa kura na kuingia katika duru ya mwisho.

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na spika wa Baraza la chini la bunge, Bw. Farmajo alipata kura 185, huku rais Mohamud akipata kura 97.

Jumla ya wabunge 328 walishiriki kwenye upigaji kura na wagombea 24 walijitosa kugombea nafasi hiyo, na watatu walijitoa kabla ya kuanza kwa upigaji kura.

No comments

Powered by Blogger.