Header Ads

Watu 73 Wauawa Kwa Bomu La Kwenye Gari Lililotegwa Na Kundi La IS Syria
Watu 73, wengi wakiwa ni waasi, wameuawa wakati kundi la IS lilipofanya shambulizi la bomu lililotegwa kwenye gari dhidi ya waasi wanaoungwa mkono na Uturuki mjini Al-Bab, Syria karibu na mipaka ya Uturuki.

Mlipuko huo ulilenga eneo la usalama la waasi katika mji wa Susian uliopo kilomita 8 kaskazini magharibi mwa mji wa Al-Bab ambao ni mji mkubwa unaoshikiliwa na kundi la IS.

Hivi karibuni Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan aliapa kuwa vikosi vya Uturuki vitaendelea kusonga kuingia katika mji mkuu wa kundi la kiislamu la Syria Raqqa, mara baada ya kukamata al-Bab.

Kujiondoa kwa IS kutoka kwa al-Bab kunakuja baada ya siku 100 ya mapigano kati ya kundi hilo na vikosi vya Uturuki na washirika waasi wa Syria.

No comments

Powered by Blogger.