Header Ads

Watu 72 Wauawa Katika Mlipuko Wa Kujitoa Mhanga Pakistan


Polisi wa Pakistan wamesema watu 72 wameuawa na wengine zaidi ya 200 wamejeruhiwa katika mlipuko wa kujitoa mhanga uliotokea jana usiku katika msikiti mmoja kwenye eneo la Sehwan mkoani Sindh, kusini mwa Pakistan.

Ofisa wa idara ya afya ya eneo la Sehwan amesema wengi waliouawa katika shambulizi hilo ni wanawake na watoto, na kutokana na idadi kubwa ya majeruhi, baadhi ya waliojeruhiwa wamekimbizwa katika hospitali mjini Hyderabad na Karachi.

Ofisa wa idara ya habari ya jeshi la Pakistan amesema jeshi la taifa limetumwa kwenye eneo la tukio kufanya kazi za uokoaji. Kamanda wa polisi eneo la Sehwan amesema mshambuliaji alijipenyeza kwenye msikiti huo na kujilipua, uliokuwa na watu 500 hadi 800. Kundi la IS limetangaza kuhusika na shambulizi hilo.

No comments

Powered by Blogger.