Header Ads

Watalii Watatu Wa China Wajeruhiwa Kwa Risasi Afrika Kusini

Watalii watatu wa China wamejeruhiwa baada ya kuporwa na genge la wahuni kwenye hoteli moja nchini Afrika Kusini.

Tukio hilo lilitokea wakati kundi la watu wanne waliokuwa na silaha, lilipovamia hoteli waliyokuwa wanafikia wachina hao kutoka mkoa wa Guangxi. Wakati wakijaribu kupambana nao, mwanamke alijeruhiwa kwa risasi kichwani, mwanaume alijeruhiwa kifuani na mguuni, na binti yao alijeruhiwa kichwani.

Ubalozi wa China nchini Afrika Kusini umetoa taarifa ukisema wahalifu walifanikiwa kukimbia na mabegi, wachina waliojeruhiwa walipelekwa hospitali na maisha yao hayako hatarini.

No comments

Powered by Blogger.