Header Ads

Wataalamu 70 Wa Huduma Kwa Wateja Kutoka Ethiopia Wamaliza Mafunzo Ya Lugha Ya Kichina

Tokeo la picha la Bole international Airport Addis Ababa

Wataalamu 70 wa huduma kwa wateja wa Ethiopia wamehitimu mafunzo ya lugha ya kichina kwa lengo la kutoa huduma bora kwa abiria kutoka China katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole huko Addis Ababa.

Mafunzo hayo yaliandaliwa na ubalozi wa China nchini Ethiopia kwa kushirikiana na chuo cha Confucius.
Wahitimu wa mafunzo hayo ni pamoja na maofisa wa forodha, maofisa wa usalama katika uwanja wa ndege wa Bole, mashirika ya ndege ya Ethiopia na ofisi ya forodha, ambao walishiriki kwenye mafunzo ya lugha ya kichina kwa muda wa wiki 10.

Balozi wa China nchini Ethiopia Bw. La Yifan na mkurugenzi msimamizi wa huduma ya uwanjani ya Ethiopia Bw. Tadele Barega wamepongeza na kuwakabidhi wahitimu hati za utambulisho katika hafla iliyofanywa katika ubalozi wa China nchini humo.

No comments

Powered by Blogger.