Header Ads

Wanawake Korea Kusini Kuishi Miaka Mingi Zaidi Duniani

Tokeo la picha la old Ladies in south korea
Wanawake nchini Korea Kusini watakuwa wa kwanza duniani kuwa na umri wa kuishi wa zaidi ya miaka 90, utafiti unaonesha.
Utafiti huo uliofanywa na Chuo cha Imperial cha London na Shirika la Afya Duniani uliangazia umri wa kuishi katika mataifa 35 yaliyostawi kiviwanda.
Utafiti huo unaonesha watu watakuwa wakishi miaka mingi kuliko sasa kufikia mwaka 2030 na pengo kati ya wanaume na wanawake litaanza kufutika katika mataifa mengi.
Watafiti hao wanasema matokeo ya utafiti wao ni changamoto kwa hazina za malipo ya uzeeni na vituo vinavyowatunza wazee.
"Korea Kusini imefanya mambo mengi kwa njia ifaayo," Prof Majid Ezzati aliambia BBC.
"Wanaonekana kuwa na mazingira yenye usawa na mambo yao mengi yamewafaa watu kwa juma - elimu, lishe - watu wengi wamenufaika.
"Na kufikia sasa, wanafanya vyema katika kukabiliana na shinikizo la damu na wana viwango vya chini zaidi vya unene duniani."
Takwimu hizo pia zinakadiria kwamba Japan, ambayo zamani ilifahamika kwa raia wake kuishi maisha marefu, inaendelea kushuka.
Kwa sasa, ina kiwango cha juu zaidi cha umri ambao wanawake huishi, lakini itapitwa hivi karibuni na KOrea Kusini na Ufaransa, utafiti huo unadokeza.
Umri wa wanaume kuishi Japan nao utashuka kutoka kuwa wa nne miongoni mwa nchi zilizochunguzwa hadi nambari 11.

No comments

Powered by Blogger.