Header Ads

Wakala Achukizwa Na Tuhuma Za Mashabiki


Wakala wa kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ujerumani Mesut Ozil amejitokea hadharani na kumtetea mchezaji wake, ambaye anakabiliwana tuhuma za kucheza chini ya kiwango.

Mashabiki wa The Gunners wanaamini Ozil anafanya kusudi kwa kucheza chini ya kiwango, hali ambayo inapelekea Arsenal kupata wakati mgumu kwenye baadhi ya michezo yake.

Dr Erkut Sogut, wakala wa kiungo huyo amesema haipendezi kwa mchezaji wake kuhusishwa na tuhuma hizo, na wakati mwingine anaamini tuhuma hizo zimekua zikimshusha na kushindwa kucheza soka la ushindani kama ilivyozoeleka.

Sogut amesema umefika wakati kwa mashabiki wa Arsenal kufahamu kuwa, mchezaji wake yupo klabuni hapo kwa maslahi ya kuisaidia The Gunners kufikia malengo na sio jambo lingine.

Kuhusu mchezo wa juzi ambapo Arsenal walikubali kipondo cha mabao matano kwa sifuri, Sogut ameeleza kuwa ni jambo la kawaida kwa timu kupoteza mchezo na wala sio mara ya kwanza kwa klabu hiyo ya London kufungwa na FC Bayern Munich, hivyo kulikua hakuan haja ya Ozil kuzongwa na tuhuma za mashabiki wanaompinga.


Ozil alianza kuibua hisia tofauti kwa mashabiki wa Arsenal, baada ya kuweka pembeni taratibu za kusaini mkataba mpya na kusisitiza hitaji la kucheza soka, huku akisubiri mustakabali wa meneja Arsene Wenger ambaye inasemekana huenda akaondoka mwishoni mwa msimu huu.

No comments

Powered by Blogger.