Header Ads

Wahamiaji 340 Wafa Maji Mwaka Huu Wakijaribu Kuingia Ulaya

Tokeo la picha la IMO - International Maritime Organization

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IMO limesema baada ya ajali ya boti iliyotokea wikiendi iliyopita, kwa jumla watu 340 wamefariki dunia katika mwaka huu wakijaribu kuingia Ulaya kupitia bahari ya Mediterranean.

Shirika hilo limeongeza kuwa vifo hivyo vimeongezeka kwa watu 250 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu, na wengi wa wahamiaji hao wanatoka Cote d'ivoire, Nigeria, Guinea, Senegal na Gambia. 

Kwa mujibu wa Shirika la Uhamiaji, baadhi ya wahamiaji waliofanikiwa kufika Ulaya wamesema safari yao ilikuwa ya hatari kuliko walivyotarajia.

Katika hatua ya kufahamisha wahamiaji hali halisi ya safari, mwaka jana IMO ikishirikiana na wizara ya mambo ya ndani ya Italia walizindua kampeni ya uelewa, ili kuwafahamisha wahamiaji kutoka nchi 15 kuhusu hatari za uhamiaji haramu kupitia jangwa la Sahara, Libya na bahari ya Mediterranean.

No comments

Powered by Blogger.