Header Ads

Wafuasi Wanne Wa Kundi La IS Washitakiwa Kwa Ugaidi Nchini Kenya

Tokeo la picha la IS Group

Watu wanne wanaotuhumiwa kuwa wafuasi wa kundi la IS wamefikishwa mahakamani mjini Mombasa, Kenya kujibu mashtaka yanayohusiana na ugaidi.

Mwendesha mashtaka wa Kenya amesema watuhumiwa hao Nasra Fais Hyder, Aisha Faiz Hayder, Salim Mohamed Rashid na Fatuma Mohammed, walikamatwa kwenye mpaka wa Uturuki na Syria wakiwa njiani kuelekea Syria, na kukabidhiwa kwa ubalozi wa Kenya nchini Uturuki.

Watuhumiwa hao wamewekwa rumande kwa siku 21 wakati polisi wakiendelea kutafuta habari zaidi kutoka kwenye simu na kompyuta zao.

Hii si mara ya kwanza kwa raia wa Kenya kukamatwa kutokana tuhuma kuwa na uhusiano na kundi la IS. Mwaka jana wanafunzi wawili walikamatwa kwa tuhuma za kuwa na uhusiano na kundi la IS.

No comments

Powered by Blogger.