Header Ads

Wafanyakazi 32 Wa Umoja Wa Mataifa Wauawa Katika Mashambulizi Mwaka Jana

Tokeo la picha la UN FLAG

Kamati ya usalama na uhuru wa huduma za kiraia za kimataifa ya Chama cha wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa imetoa taarifa ikisema wafanyakazi zaidi ya 32 wa umoja huo waliuawa katika mashambulizi ya makusudi mwaka jana, wengi wao wakiwa ni walinzi wa amani.

Naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa Bw. Farhan Haq amesema, waliouawa ni pamoja na walinzi wawili wa usalama, mfanyakazi wa kiraia na mkandarasi mmoja.

Katika miaka mitano iliyopita, wafanyakazi karibu 240 wa umoja huo waliuawa katika mashambulizi ya makusudi.

No comments

Powered by Blogger.