Header Ads

Vyama Vikubwa Vya Upinzani Kenya Kuweka Mgombea Mmoja Wa Urais

Tokeo la picha la Kalonzo Musyoka

Viongozi wa vyama vikubwa vya upinzani vya Kenya wamekubaliana kuweka mgombea mmoja wa urais, na kutoa mwito kwa vyama vyote kuwa makini kuhakikisha kuwa hakuna njama za kufanya udanganyifu kwenye uchaguzi.

Hata hivyo muungano mpya mkubwa wa upinzani unaojulikana kama NASA haukutaja jina la mgombea wake, kuwa wanasheria na wataalamu wake wamekuwa wakiandaa makubaliano kuhusu namna ya kugawana madaraka.

Aliyekuwa makamu wa Rais wa Kenya Kalonzo Musyoka amesema muungano mpya wa wapinzani una nguvu mpya, na unaoongozwa kwa kanuni ya nia njema. 

Muungano huo unaundwa na vyama vya ODM kinachoongozwa na Raila Odinga, FORD-Kenya kinachoongozwa na Bw Moses Wetangula, ANC kinachoongozwa na Bw Musalia Mudavadi na WIPER kinachoongozwa na Bw Musyoka

No comments

Powered by Blogger.