Header Ads

UNHCR Yatahadharisha Kuhusu Wimbi Kubwa La Wakimbizi Wa Sudan Kusini Wanaokimbilia Sudan

Tokeo la picha la UNHCR

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limetoa tahadhari kuhusu ongezeko kubwa la watu wa Sudan Kusini wanaokimbilia Sudan tangu mwanzo wa mwaka huu.

Makadirio ya awali ni kuwa wakimbizi elfu 60 wanaweza kuingia Sudan mwaka huu, lakini katika miezi miwili iliyopita, wakimbizi zaidi ya elfu 31 wamekimbilia nchini humo.

Inakadiriwa kuwa zaidi ya asilimia 80 ya wakimbizi wapya ni wanawake na watoto wakiwemo watoto walio peke yao na waliotengana na familia zao.

Sudan ni moja ya nchi majirani za Sudan Kusini zinazopokea mawimbi makubwa ya wakimbizi kutoka Sudan Kusini. Zaidi ya wakimbizi milioni 1.5 kutoka Sudan Kusini wamekimbilia nchi majirani za kanda hiyo, na nusu yao wameingia Uganda.

No comments

Powered by Blogger.