Header Ads

Umoja Wa Mataifa Walaani Shambulio La Msikiti Nchini Canada


Umoja wa Mataifa umelaani shambulizi la kigaidi lililotokea kwenye msikiti mmoja huko Quebec, nchini Canada, ambapo watu sita waliuawa.

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja huo Stephane Dujarric amesema, Umoja huo unafuatilia maendeleo ya uchunguzi wa shambulizi hilo la kutisha, na kulaani shambulizi hilo la kigaidi kwenye sehemu ya kuabudu.

Amesema anatumai kuwa serikali na wananchi wa Canada wataungana katika kupinga jaribio lolote la kupanda mbegu ya utengano kwa msingi wa kidini.


Dujarric pia ametoa salamu za rambirambi kwa familia za watu waliouawa kwenye shambulizi hilo, na kuwatakia majeruhi afya njema.

No comments

Powered by Blogger.