Header Ads

Umoja Wa Mataifa Waingiwa Hofu Juu Ya Uhaba Wa Maji Mjini Aleppo, Syria

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric jana alieleza wasiwasi wa umoja huo juu ya uhaba wa maji unaoathiri watu takriban milioni 1.8 mjini Aleppo na sehemu zilizoko karibu nchini Syria.

Amesema kuwa ili kukabiliana na hali hiyo, Umoja wa Mataifa imetoa mafuta kuwezesha pampu za maji kuendelea kuvuta maji kutoka kwenye visima 100 vya kina kirefu na kusaidia kusambaza maji kwa watu karibu milioni 1. 

Msemaji huyo pia amsema Umoja wa Mataifa unataka pande mbalimbali za nchi hiyo kuhakikisha vifaa vya misaada vinafikishwa kwa watu wenye mahitaji kote nchini humo bila vizuizi na bila masharti.

Habari nyingine zinasema kuwa siku hiyohiyo kundi la IS limelipua mabomba ya gesi kwenye kisima cha gesi cha Hayan mkoani Homs na kusababisha moto mkubwa.

Hadi sasa, mgogoro wa Syria umesababisha vifo vya watu zaidi ya laki 3 na wengine takriban milioni 11 kuwa wakimbizi.

No comments

Powered by Blogger.