Header Ads

Umoja Wa Mataifa Na Wadau Wa Amani Wataka Utekelezaji Kamili Wa Makubaliano Yaliyofikiwa Disemba 31 Nchini DRC

Tokeo la picha la CONGO RDc flag

Mashirika manne ya kimataifa ikiwemo Umoja wa Mataifa yameeleza wasiwasi wao kuhusu kuchelewa kwa utekelezaji wa makubaliano ya kisiasa yaliyofikiwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Disemba 31 mwaka jana.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa na Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, na Jumuiya ya Nchi zinazotumia lugha ya Kifaransa (IOF) imesema, pande husika nchini DRC bado hazijamaliza majadiliano kuhusu njia za kutekeleza makubaliano hayo. 

Taarifa imesema, hali hiyo inweza kudhoofisha nia njema ya kisiasa iliyosaidia kusainiwa kwa makubaliano hayo.

Makubaliano yaliyofikiwa mwezi Desemba mwaka jana yanamzuia rais wa sasa Joseph Kabila kugombea nafasi ya urais kwa kipindi cha tatu, na pia yanaelekeza kuwa na kipindi cha mpito kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huru na wa amani mwishoni mwa mwaka huu.

No comments

Powered by Blogger.