Header Ads

Uingereza Yasherehe Miaka 65 Ya Utawala Wa Malkia Elizabeth II


Malkia Elizabeth II wa Uingereza ameadhimisha miaka 65 tangu aanze kutawala nchi hiyo.

Kikundi cha askari wa farasi wa mfalme wa Uingereza kilitoa heshima kwa Malkia huyo mjini London, idara ya kutengeneza sarafu ya kifalme ya Uingereza na idara ya posta ya kifalme pia zilichapisha sarafu za kumbukumbu na stampu ili kusherehekea siku hiyo.

Malkia Elizabeth II alitawazwa kuwa Malkia wa Uingereza tarehe 6 mwezi Februari mwaka 1952 baada ya kufariki kwa baba yake Mfalme George VI, wakati huo akiwa na miaka 25. 

Mpaka sasa ameshuhudia mabadiliko ya mawaziri wakuu 12 wa Uingereza, na alidumu katika kiti cha mfalme kwa muda mrefu zaidi duniani.

No comments

Powered by Blogger.