Header Ads

Uingereza Yaipatia Rwanda Paundi Milioni 5 Kuendeleza Sekta Ya Kilimo

Tokeo la picha la rwanda

Rwanda na Idara ya maendeleo ya kimataifa ya Uingereza DFID wamesaini makubaliano yenye thamani ya paundi milioni 5 kwa ajili ya mageuzi ya kilimo nchini Rwanda.

Kiongozi wa Ofisi ya DFID nchini Rwanda Laure Beaufils ametoa wito kwa serikali kuhakikisha mageuzi ya kilimo yanafanyika kwa ufanisi ikiwa sambamba na juhudi za kupunguza athari za mabalidiko ya hali ya hewa.

Beaufils amesema kilimo ni sekta muhimu katika ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini, na Uingereza itaendelea kuunga mkono maendeleo ya Rwanda. Ametaka fedha hizo zitumike kuhimiza uzalishaji wa kilimo na kuwanufaisha watu maskini.

Waziri wa fedha wa Rwanda Claver Gatete amesema fedha hizo zitahakikisha ukuaji endelevu kwenye uzalishaji wa kilimo nchini Rwanda.

No comments

Powered by Blogger.