Header Ads

Theresa May: Baraza La Juu La Bunge La Uingereza Lisijaribu Kuzuia Mchakato Wa Kujitoa Umoja Wa Ulaya

Tokeo la picha la Theresa May

Baraza la juu la bunge la Uingereza lilifanya majadiliano ya siku mbili kuhusu muswada uliotolewa na serikali ya Uingereza kuhusu Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya. 

Waziri mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May siku hiyo aliwasisitiza wabunge kuheshimu nia ya wananchi na wasijaribu kuzuia mchakato wa Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya kwa.

Tarehe 8 mwezi huu baraza la chini la bunge la Uingereza liliupiga kura mswada wa kujitoa Umoja wa Ulaya na liliunga mkono mswada huo kwa kura 494 za ndiyo na kura 122 za hapana. 

Muswada huo umewasilishwa kwenye baraza la juu la bunge la Uingereza kwa ajili ya majadiliano. Lakini vyama vya upinzani na wabunge kadhaa walitaka kutafuta mswada wa marekebisho ili kuahirisha wakati wa kuanzisha mchakato wa kujitoa.

No comments

Powered by Blogger.