Header Ads

Syria Yaitaka Uturuki Kuondoa Jeshi Lake Kutoka Syria Na Kufunga Mpaka Kati Ya Nchi Mbili

Tokeo la picha la Syria And turkey

Serikali ya Syria imeitaka Uturuki iondoe jeshi lake kutoka Syria na kufunga mipaka kati ya nchi mbili ili kuzuia magaidi wasiingie nchini humo. 

Mjumbe wa serikali ya Syria kwenye mazungumzo ya Astana Bashar al-Ja'afari ameituhumu Uturuki kwa kuvamia ardhi ya Syria na kusema imeshindwa kutekeleza wajibu wake na kuruhusu maelfu ya mamluki kutoka nchi mbalimbali kuingia Syria kupitia mpaka wa nchi hizo mbili.

No comments

Powered by Blogger.