Header Ads

Space X Yarusha Roketi Kupeleka Vifaa Kwenye Kituo Cha Anga Cha ISS


Kampuni ya teknolojia ya anga ya juu ya Marekani Space X imerusha kwa mafanikio roketi yake ya 10 ya kupeleka vifaa kwenye kituo cha anga za juu cha kimataifa ISS mapema jana kutoka kwenye kituo cha kurushia vyombo vya anga za juu cha Kennedy, ukiwa ni urushaji wa kwanza wa kibiashara kufanywa na Space X. 

Dakika nane baada ya kurushwa, sehemu ya kwanza ya roketi hiyo ilirudi salama kwenye jukwaa lake lililoko pwani ya Florida.

No comments

Powered by Blogger.