Header Ads

Shirika La Ndege La Ethiopia Lachukua Nafasi Ya Juu Kwa Kutochelewa


Shirika la ndege la Ethiopia ambalo ni shirika kubwa zaidi la ndege barani Afrika limechukua nafasi ya 11 duniani kwenye hali ya kutochelewesha safari za ndege katika mwezi wa Januari.

Kwa mujibu wa kampuni ya data za safari za ndege ya FlightStats, kati ya safari karibu elfu nane za ndege za shirika hilo kwa mwezi wa Januari, asilimia 81 yao zilifika ndani ya dakika 15 kwa kufuata ratiba.

Shirika la ndege la Ethiopia pia linachukua nafasi ya kwanza kwa kutochelesha safari za ndege katika Mashariki ya Kati na barani Afrika.

No comments

Powered by Blogger.