Header Ads

Serikali Ya Burundi Kuhudhuria Mazungumzo Nchini Tanzania

Tokeo la picha la Willy Nyamitwe

Ofisi ya rais wa Burundi jana imethibitisha serikali ya Burundi itahudhuria mazungumzo ya kusaka suluhu yatakayofanyika tarehe 16 hadi 18 mjini Arusha, Tanzania.

Ofisa mawasiliano wa rais wa Burundi Willy Nyamitwe amesema wananchi wa Burundi kutoka vyama tofauti vya siasa au jamii, vyombo vya habari au makundi ya kidini watakutana ili kutafuta ufumbuzi wa masuala yanayoikabili Burundi. 

Amsema serikali ya Burundi itaunga mkono mazungumzo yoyote yanayolenga kutatua matatizo.

Rais wa zamani wa Tanzania  Benjamin Mkapa amesema mazungumzo hayo yatafuatilia masuala halisi, na hatimaye makubaliano yatafikiwa. Bw. Mkapa ametoa wito kwa vyama vyote kusitisha mapambano ili kutoa nafasi kwa mazungumzo hayo yatakayomalizika Mwezi Juni mwaka huu.

Hata hivyo kundi la upinzani la Burundi CNARED, limesema halitashiriki kwenye mazungumzo hayo.

No comments

Powered by Blogger.