Header Ads

Sergio Aguero Amuweka Njia Panda Pep Guardiola

Tokeo la picha la pep guardiola and kun

Meneja wa Man City Pep Guardiola, ameonyesha kutokua na uhakika wa kuendelea kufanya kazi na mshambuliaji kutoka nchini Argentina Sergio Aguero.

Guardiola ambaye ameshindwa kumtumia mshambuliaji huyo katika kikosi cha kwanza, amewaambia waandiahi wa habari hana uhakika kama mshambuliaji huyo ataendelea kuwa sehemu ya kiksoi chake, itakapofika mwishoni mwa msimu huu.

Guardiola aliwaambia waandishi wa habari suala hilo, apoulizwa uwezekano wa kuendelea kufanya kazi na Aguero, ambaye amekua na wakati mgumu wa kucheza katika kikosi cha kwanza tangu aliposajiliwa mshambuliaji kutoka nchini Brazil Gabriel Jesus.

Guardiola alisema: “Sijui kama hilo litatokea.

“Sergio anajua msimamo wa bosi wake. Sitakia kumuweka sokoni, nataka aendelea kuwa sehemu ya kikosi changu kwa kipindi chote nitakachokua hapa.

“Wakati Sergio alipofungiwa kucheza michezo saba tulimiss, lakini mambo mengine yaliendelea kwa wachezaji mbadala kucheza sehemu yake.

“Siwezi kusema mambo mengi kuhusu yeye, lakini sina uhakika wa mustakabali wake japo ninatamani kuendelea kufanyana nae kazi.


“Sijui nini kitakachotokea kesho, natambua ana mawazo yake binafsi na katu hapaswi kuingiliwa, ila bado msimao wangu upo pale pale, nataka kumuona akiendelea kuwa hapa."

No comments

Powered by Blogger.