Header Ads

Roy Keane: Arsenal Walistahili Kipigo Cha Paka Mwizi

Tokeo la picha la Roy Keane on ITV 2017

Gwiji wa klabu ya Man Utd Roy Keane ameipiga kijembe Arsenal kwa kusema haikuwa tayari kupamba na mabingwa wa soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich.

The Gunners walichapwa mabao matano kwa moja usiku wa kuamkia leo, kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya 16 ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Roy Keane alipiga kijembe hicho alipokua akizungumzia matokeo ya mchezo huo, wakati wa kuhitimisha uchambuzi wake kupitia televisheni ya ITV.

"Sikushangazwa na kilichotokea," Alisema Keane.

"Ulidhani watakwenda Munich na kupata matokeo mazuri mbele ya Bayern Munich?

"Janga hili lilitabiriwa kabla, huwezi kushinda mchezo muhimu na mzito kama huu, ukiwa na viongozi dhaifu na wachezaji wavivu.


"Hiki ndicho Arsenal walistahili kukipata, ukiangalia matokeo ya michezo kadhaa waliyocheza, inakupa taswira ya matokeo waliyoyapata mjini Munich. Aliongeza Keane.

No comments

Powered by Blogger.