Header Ads

Real Madrid Watamba Nyumbani

Real Madrid's Karim Benzema celebrates scoring against Napoli

Mabingwa watetezi wa ligi ya mabingwa barani Ulaya Real Madrid wamejiweka katika hatua nzuri ya kuendelea kutetea ubingwa wao, kwa kufanikisha ushindi wa mabao matatu kwa moja dhidi ya SSC Napoli.

Wakicheza kwenye uwanja wa nyumbani wa Santiago Bernabeu, Real Madrid walitanguliwa kufungwa na wageni wao katika dakika ya nane ambapo bao la SSC Napoli lilikwamishwa kimiani na Lorenzo Insigne.

Mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa Karim Benzema aliisawazishia Real Madrid katika dakika ya 18, kabla ya Toni Kroos na Casemiro hawajaongeza bao la pili na la tatu katika dakika ya 49 na 54.


Real Madrid watalazimika kuulinda ushindi huo watakapokwenda mjini Naples nchini Italia majuma mawili yajayo, ili kujihakikishia nafasi ya utetezi wa ubingwa wa michuano ya barani Ulaya msimu huu.

No comments

Powered by Blogger.