Header Ads

RC Makalla Akutana Na Vikundi Vya Ufugaji Kuku Vinavyofadhiliwa Na Taasisi Ya BRAC
Mkuu wa mkoa Wa Mbeya Mh.Amos Makalla akizungumza na baadhi ya akina mama wa jijini Mbeya wanao kopeshwa na Taasisi ya Mfuko wa Uwekezaji Mradi (BRAC) jijini Mbeya.


RC Makalla ameipongeza taasisi hiyo kwa kuvikopesha vikundi hivyo vya ujasiliamali,dhamira kuu ikiwa ni vikundi hivyo kuongeza uzalishaji wa Mahindi na ufugaji wa kuku kwa wingi.Taasisi ya BRAC imevikopesha vikundi vipatavyo 20 kiasi cha shilingi milioni 770 kwa ajili kuendeleza miradi yao mbalimbali ikiwemo ya ufugaji kuku na kilimo

RC Makalla pia amewaagiza maafisa Ugani kuwatembelea Wafugaji na wakulima mara mara ili kuwapa maelekezo namna ya kuiendeleza na kuisimamia vyema miradi yao mbalimbali,ambayo imekuwa ikiwapatia kipatao na kuendelea kujikwamua katika suala zima la kupambana na umaskini

"nimefurahishwa sana na juhudi zenu za ujasiliamali,hakika ndio njia nyingine mbadala ya kujiingizia kipato na kuhakikisha suala la umaskini linakuwa historia miongoni mwenu,hivyo nawapongeza sana na msikate tamaa"alisisitiza RC Makalla huku akiongeza kwa kuwataka Wananchi kufanya kazi,kwani maendeleo hayaji kwa watu kukaa na kuyasubiri bila kufanya jitihada zozote.Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Amosi Makalla akiwa katika picha ya pamoja ya viongozi wa Taasisi ya Mfuko wa Uwekezaji Mradi (BRAC) na baadhi ya Wajasiliamali kutoka katika vikundi vipatavyo 20 vya jijini Mbeya.Baadhi ya kuku wa kienyeji wanaofungwa na vikundi hivyo vya ujasiliamali mkoani Mbeya.Baadhi ya akina Mama Wajasiliamali wanaounda vikundi 20 wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Amos Makalla alipokuwa akizungumza nao mara baada ya kuwatembelea kwenye maeneo ya miradi yao wanayoiendeleza baada kukopeshwa fedha na taasisi ya BRAC

No comments

Powered by Blogger.