Header Ads

Rais Wa Uganda Kutembelea Bandari Ya Dar es Salaam

Tokeo la picha la museveniRais Yoweri Museveni wa Uganda anatarajiwa kutembelea bandari ya Dar es Salaam Tanzania tarehe 26 mwezi huu, kuangalia marekebisho yaliyofanyika ili kuhamasisha wafanyabiashara wa Uganda waanze kutumia tena bandari hiyo. 

Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Dk Augustine Mahiga amesema, rais Museveni ataanza ziara ya siku mbili nchini Tanzania Jumamosi, ambapo marais wa nchi hizo mbili watakutana kujadili uhusiano na ushirikiano kati ya nchi mbili katika sekta za biashara, nishati na uchukuzi.

No comments

Powered by Blogger.