Header Ads

Rais Wa Sudan Amwachia Huru Mwanahabari Wa Czech Aliyefungwa

Tokeo la picha la Omar al-Bashir

Rais Omar al-Bashir wa Sudan ametoa msamaha kwa mwanahabari wa Czech Petr Jasek baada ya mahakama ya nchi hiyo kumhukumu kifungo cha miaka 20 kwa mashtaka ya ujasusi dhidi ya nchi hiyo.

Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Bw. Ibrahim Ghandour amesema, rais al-Bashir amemwachia mwanahabari huyo ili kuheshimu uhusiano kati ya Sudan na Jamhuri ya Czech.

Bw. Ghandour amesema hayo baada ya kukutana na mwenzake wa Jamhuri ya Czech Bw. Lubomir Zaoraleka ambaye yuko ziarani nchini Sudan.

Bw. Lubomir Zaoralek ameeleza kuridhika na matokeo ya tukio hilo, na kusema atampokea mwanahabari huyo atakayerudi nyumbani.

No comments

Powered by Blogger.