Header Ads

Rais Wa Somalia Aapa Kuongeza Mapambano Dhidi Ya Al-Shabaab

Tokeo la picha la Mohamed Abdullahi Mohamed

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed ambaye anajulikana zaidi kama Farmajo, ameahidi kushirikiana na tume maalumu ya Umoja wa Afrika katika kupambana na kundi la kigaidi la Al-Shabaab ili kuleta utulivu nchini humo.

Farmajo alisema hayo kwenye mkutano na viongozi wa Umoja wa Afrika na mabalozi wa vikosi vinavyochangia kusimamia usalama (TCC) mjini Mogadishu.

Vilevile ameeleza kuwa, matumaini yake katika miaka miwili ijayo ni kuwashinda Al-Shabaab na kusema hayo yanawezekana endapo nchi wanachama wa Umoja wa Afrika watashirikiana pamoja.

Wakati huo huo kikosi cha kupambana na ugaidi nchini Kenya, kimewakamata watu wawili wanaosadikiwa ni wa kundi la IS mjini Mombasa wakati wa msako wa kuwakamata vijana waliojiunga na makundi ya watu wenye siasa kali toka nje ya nchi hiyo.

Kamanda wa polisi wa kaunti ya Mombasa Peter Maelo amesema, watuhumiwa wawili hao wanahojiwa ili kuwezesha kupata taarifa zaidi juu ya mtandao wa kigaidi nchini Kenya.

No comments

Powered by Blogger.