Header Ads

Rais Wa Marekani Awapigia Simu Marais Wa Afrika Kusini Na Nigeria

Tokeo la picha la trump Phone

Rais Donald Trump wa Marekani jana aliwapigia simu rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria. 

Kwenye mazungumzo rais Zuma alimpongeza Trump kwa kuchaguliwa kuwa rais na wamekubali kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano kati ya nchi mbili haswa kwenye kuhimiza amani na utulivu barani Afrika. 

Akiongea na rais Buhari wa Nigeria, Rais Trump alimhakikishia kuwa Marekani inaandaa mpango mpya wa kutoa vifaa vya kijeshi kwa Nigeria ili kuisaidia kupambana na ugaidi.

No comments

Powered by Blogger.