Header Ads

Rais Wa Marekani Akutana Na Mjumbe Wa Taifa Wa China

Tokeo la picha la Donald Trump and Yang Jiech

Rais Donald Trump wa Marekani amekutana na mjumbe wa taifa wa China Bw. Yang Jiechi ambaye yuko ziarani nchini Marekani, na kufanya naye mazungumzo kuhusu uhusiano wa pande mbili.

Bw. Yang amesema mazungumzo kwa njia ya simu yaliyofanywa na marais wa nchi hizo mbili yana umuhimu mkubwa, na yametoa mwelekeo wa maendeleo ya uhusiano kati ya China na Marekani katika kipindi kijacho.

Rais Trump amesema, alifurahia kuongea na rais Xi kwa njia ya simu, na kusema Marekani inatilia maanani uhusiano kati yake na China, pande mbili zinatakiwa kuimarisha mawasiliano ya viongozi, kuzidisha ushirikiano katika sekta mbalimbali na kuimarisha uratibu katika mambo ya kikanda na kimataifa.

No comments

Powered by Blogger.